Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Champion Boy’ usiku wa Ijumaa timu yake ya KRC Genk ikiambulia kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya wenyeji Standard Liege anayecheza mchezaji toka Uganda Frank Miya mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji uliopigwa kwenye uwanja wa Maurice Dufrasne Mjini Liege.Samatta jana alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 41 ikiwa ya tano tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya Jamhuri ya Kisemokrasia ya Kongo (DRC) na bahati nzuri kwake hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu na huu ulikuwa mchezo wao wa pili wa Ligi hiyo msimu huu kwani mechi ya kwanza walitoka sare ya 3-3 na Waasland-Beveren Uwanja wa nyumbani, Luminus Arena.
Katika mchezo huo, Genk walitangulia kupata bao, lililofungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 21, Siebe Schrijvers dakika ya 36, kabla ya kiungo Mbrazil Edmilson Junior kuwasawazishia wenyeji dakika ya 48 na mshambuliaji Mkongo, Paul-Jose M’Poku Ebunge kufunga la ushindi dakika ya 63.

Post a Comment

 
Top