Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Bado kesi ya Mwigizaji Wema Sepetu kuhusu bangi inaendelea kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam ambapo leo ilikua ni siku nyingine tena kesi hiyo imeendelea.
Mpya ya leo ni kwamba Mahakama hiyo imekataa kupokea vielelezo vya ushahidi wa msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Wema na wenzake.Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema Mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro  “Nakubaliana na hoja kwamba msokoto wa bangi na vipisi vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua Mahakamani“
Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.

Post a Comment

 
Top