Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Tupo mwishoni mwa mwaka, anyway nimependa kukusogezea tukio muhimu lilopata kutingisha kwa mwaka huu. Tukio hilo ni kuvishana pete kwa mastaa mbalimbali bila ndoa 2016.

List ya tukio hili ni ndefu kutokana na kuwepo kwa jambo hili kwa mastaa wengi sana. Hapa nimeweza kukusogezea list fupi ya mastaa kutoka mbele.
Hii hapa list ya mastaa 5 wa mbele ambao walivalishana pete kwa lengo la kuoana, lakini ndoto zao hizo hazikukamilika hadi kufikia leo hii ambapo tunazidi kuelekea mwishoni mwa mwaka huu.
Orodha nzima hii hapa
 1. Mariah Carey & James PackerImage result for Mariah Carey & James Packer
  Taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii duniani zilienea habari za nyota wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey kuvishwa pete ya uchumba na mpenzi wake, bilionea James Packer raia wa nchini Australia.
  Uhusiano wa wawili hao ulianza tangu 2015 mara baada ya Mariah kuachana na baba watoto wake Nick Cannon, ambaye alifanikiwa kupata naye watoto wawili mapacha, hivyo kuachana kwao kulimpa nafasi mfanyabiashara huyo kutoka nchini Australia kuonesha jeuri ya fedha.
  Hawakuchelewa kuonesha uhusiano wao, hivyo James aliamua kununua pete ya dhahabu yenye thamani ya zaidi ya bilioni 21 za Kitanzania, hapo hapo kutangaza ndoa ambayo waliweka wazi kuwa kabla ya mwaka 2016 kumalizika watakuwa wamefunga.
  Wengi walikuwa wanaisubiri ndoa hiyo kwa hamu kutokana na fedha zilizotumika kwenye kununua pete, lakini mambo yalikuwa tofauti siku chache baadaye, ambapo ndoto za wawili hao za kufunga ndoa mwaka huu zikafikia mwisho mwezi Oktoba. Kwa sasa wamebaki kuwa na mgogoro wa kupotezana muda.
  2. Blac Chyna & Rob KardashianImage result for Blac Chyna & Rob KardashianBlac Chyna ni mwanamitindo maarufu nchini Marekani ambaye alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza akiwa na uhusiano na rapa Tyga, lakini Januari mwaka huu aliweka wazi kuwa anatoka na kaka wa Kim Kardashian, Rob Kardashian.
  Aprili mwaka huu, mrembo huyo alivishwa pete na mchumba huyo huku wakitangaza kutaka kufunga ndoa Desemba mwaka huu mara baada ya kufanikiwa kupata mtoto wao, kwanza walianza kwa kufanikiwa kupata mtoto mapema Novemba na ndipo watu wakawa wanasubiri ndoa ya wawili hao Desemba.
  Kwa sasa imebaki stori kwa kuwa wawili hao tayari wameachana mapema Desemba hii kwa madai kwamba familia ya Rob amekuwa na michepuko mingi, hataki ushauri kutoka kwa mrembo, pamoja na migogoro ambayo inaendelea ndani ya familia hiyo ya Kardashian, kwa sasa kila mmoja anaishi kivyake japokuwa wakiwa na mtoto wa mwezi mmoja.
  3. Nicki Minaj & Meek MillImage result for Nicki Minaj & Meek Mill
  Wawili hao wanafanya muziki wa Hip Hop nchini Marekani, walianza uhusiano wao tangu 2015, lakini mapema mwaka huu walitangaza kutaka kufunga ndoa mara baada ya Meek Mill kumvisha pete mchumba huyo.
  Mapema Novemba mwaka huu kulikuwa na taarifa kwamba wawili hao wameachana, lakini hakuna ukweli huo, bado wapo pamoja na wanaendelea na ratiba yao ya kutaka kufunga ndoa.
  Ukweli ni kwamba dalili za ndoa hiyo kufanyika mwaka huu hazipo baada ya hivi karibuni kuripotiwa kuwa wameachana, hivyo kwa wiki hii moja iliyobaki kuingia 2017 ni asilimia chache wawili hao kurudiana na hatimae kufunga ndoa.
  4. Miley Cyrus & Liam HemsworthImage result for Miley Cyrus & Liam Hemsworth
  Wawili hao ni wapenzi wa muda mrefu tangu 2012, na wamekuwa wakiachana na kurudiana ambapo ni zaidi ya mara mbili sasa, lakini Januari mwaka huu waliweka wazi kuwa wanataka kufunga ndoa lakini cha kushangaza hadi sasa dalili za kufunga ndoa hazipo kabisa wamebaki kuvishana pete.
  5. Jason Statham & Rosie WhiteleyImage result for Jason Statham & Rosie Whiteley
  Hao ni nyota wa filamu, wamekuwa kwenye uhusiano wa wazi tangu 2010, lakini mapema mwaka huu Statham alifanikiwa kumvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambapo hafla hiyo ilifanyika nchini Thailand, lakini hadi sasa kimya hakuna dalili zozote za ndoa yao.

Post a Comment

 
Top