Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva asiyeishiwa vituko kila kukicha, Harmorapa ‘Mr Kiki’, ameachia ngoma mpya inayoitwa Ajitokeze ambapo ndani yake kuna mistari ambayo mashabiki wanadai amemtupia dongo meneja wake wa zamani, P Funk Majani.
“Nishakuwa mfagizi chini ya miti, nazijua kero za majani, maana majani hayafadhiliki, ndiyo maana sipatani na majani”
Hiyo ndiyo mistari inayopatikana kwenye ngoma ya Ajitokeze, ambayo mashabiki wanadai kwamba kutokana na Harmorapa kutimuliwa na meneja wake huyo, ndiyo iliyosababisha amtungie mistari hiyo ya kumdiss.
Juhudi za kumsaka Harmorapa, na kumsomea shtaka la kumdiss meneja wake wa zamani kwenye ngoma yake mpya, zilizaa matunda na alitoa majibu yafuatayo.

“Ni kweli kwa sasa P Funk Majani siyo meneja wangu, ila siyo kweli kwamba nimemdiss kwenye ngoma yangu, kwa sababu hatuko pamoja kikazi ila bado tuna mahusiano mazuri na hatuna ugomvi, wala hajawahi kunitimua hizo ni fununu tu.Ngoma yangu ya Ajitokeze ni ngoma inayonizungumzia mimi, kwamba hakuna anayeweza kutokea akawa kama mimi na kama yupo basi ajitokeze, ila siyo dongo kwa Majani,” amesema Harmo Rapa.

Post a Comment

 
Top