Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hamisa enzi za ujauzito
Mwanamitindo maarufu ambaye pia ni muuza nyago kunako video za wasanii Bongo, Hamisa Mobbeto,amejifungua mtoto wa kiume leo.Ubuyu wa Hamisa kujifungua umezagaa mitandaoni baada ya mama yake mzazi kuposti picha ya mkono wa mtoto na kuandika maneno yafuatayo.
“Alhamdullilah mume wangu miye peke yangu”
Baada ya posti hiyo ya mama yake mzazi, saa chache baadaye Hamisa alithibitisha taarifa hizo kwa kuposti picha ya mtoto wake na kuandika ujumbe ufuatao.
“Ahsante Mungu, Karibu duniani mshindi”
Hamisa ni mzazi mwenza wa mfanyabiashara maarufu, Majizzo, aliyezaa naye mtoto wa kwanza anayeitwa Fantasy, ambapo mpaka sasa hajaweka wazi ni nani baba wa mtoto wake huyu wa pili.

Post a Comment

 
Top