Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii na Video vixen maarufu Bongo, Gift Stanford 'Giggy Money' amefunguka na kudai kuwa mara nyingi kinachomfanya ajitoe ufahamu na kufanya vitu vya ajabu hadharani ni kutokana na kile anachokiita 'stress' za mapenzi.Akizungumza hivi karibuni Giggy amesema kuwa matukio hapa katikati yaliyotokea na mengi ya kudhalilisha ikiwepo kujirekodi video akiwa na Mwanasheria Albert Msando ni kutokana na mapenzi yalivyokuwa yakimchanganya hasa matukio ya kumfumania mpenzi wake wakati mbele za watu mpenzi wake huyo anaonekana ni mpole.Unajua wakati nafanya drama zangu watu walikuwa hawanielewi sana. Watu wananiona mimi nafuraha kila wakati lakini mimi moyoni mwangu najua nini ambacho kinaniumiza. Wakati narekodi video na Msando tayari nimeshavurugwa vya kutosha. Hata jinsi ambavyo nimepungua japo ni ukuaji lakini pia mawazo ya mapenzi yalikuwa yananisumbua sana" alisema.
Unajua niliwahi kumfumania mpenzi wangu akiwa na rafiki yangu kitandani lakini nikamwambia hebu vaa nguo twende. Siyo kitu rahisi kwa mwanamke kufanya kitu kama hicho. Ni bora kuwa na mwanaume ambaye unajua ni kicheche au mlevi kuliko mwanaume mpole ambaye kainamisha kichwa kumbe huko nyuma anamambo makubwa kabeba
Akizungumzia kuhusu warembo ambao wanapiga picha za utupu na kuziweka mitandaoni kwa kumuiga yeye Giggy amesema kutengeneza jina siyo lazima mpaka picha za utupu kwani wakati mwingine zina madhara.

"Watu wanahisi kuwa mimi nimetoboa kirahisi, ukweli mimi nimepata tabu sana na pia imenifanya nishindwe kupata hata madili makubwa makubwa kutokana na muonekano lakini sasa ma video vixen wengi ni wachafu na hawajui hilo. Wasiige vitu ambavyo hawaviezi kwa sababu tu Giggy anafanya" aliongeza.

Post a Comment

 
Top