Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Darasa akikamua
IMEFIKA! Baada ya kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi, hatimaye wakali wawili wasioshikika kunako gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ na Sharif Thabeet ‘Darassa’ leo Jumamosi wanatarajiwa kuweka historia mpya kwa kupiga bonge moja la shoo katika uzinduzi wa hoteli ba’kubwa ya JS Motel iliyopo Chato Mjini mkoani Geita.
DarassaAkizungumza na Championi Jumamosi, Darassa anayebamba na Ngoma ya Hasara Roho pamoja na ngoma ya taifa ya Muziki alisema kuwa, kwa mara nyingine anarudi Chato lakini safari hii anarudi kuonyesha burudani ya kishindo zaidi kwa kuwa itawahusisha wateja na waalikwa wote watakaofika katika uzinduzi wa JS Motel.
“Huwa sikosei linapotokea suala la mualiko kama hili la uzinduzi. Nashukuru kuwa miongoni mwa watakaozindua JS Motel ndani ya Chato Mjini kwa mara ya kwanza na ninachoahidi ni kufanya makamuzi ya ‘live’ jukwaani nikipiga nyimbo zangu zote ikiwemo Too Much, Sikati Tamaa, Weka Ngoma pamoja na ngoma yetu hii ya taifa ya Muziki,” alisema Darassa.
Snura
Kwa upande wa Snura ama Mamaa Majanga kama wengi wanavyomuita alisema, siku hiyo ya uzinduzi atafanya tukio ambalo si la nchi hii kutokana na alivyojiandaa pamoja na madansa wake.
Snura
“Mashabiki wote wanaifahamu shughuli yangu nikiwa katikati ya jukwaa. Tena hii imekuja mahala pake kwani nitawazindulia ngoma yangu mpya hukohuko kwenye uzinduzi wa JS Motel, asikwambie mtu yaani nitakinukisha mwanzo mwisho, kuanzia Chura, Najibadua, Shindu, Ushaharibu, Majanga na nyingine kibao.
“Siku hiyo sitawaimbia tu, nitawapa staili mpya ya kucheza nyimbo hizo ikiwemo na ya sasa ya Nionee Wivu niliowashirikisha Yamoto Band,” alisema Snura ambaye atakuwa na timu yake nzima ya madansa namba moja kwa kukata ‘uno’ jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top