Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wanajeshi wa Kenya wakituliza ghasia
WAKENYA katika matabaka mawili tofauti wameandamana barabarani! Tabaka la kwanza ni lile la raia wa kawaida, hawa wanayapinga matokeo ya urais yanayotangazwa wakiwa na hoja kwamba, matokeo yalidukuliwa. Wengi wa waandamanaji wanaamini Raila mwana wa Odinga alistahili kuibuka kidedea! Wameamua kurandaranda barabarani wakiimba nyimbo za kuhamasishana mpaka kieleweke!
CHONDECHONDE WAKENYA!
Tabaka la pili lililotandaza mbawa zake ni lile la askari watiifu, ambao wao wamesimama barabarani kwa ajenda moja tu; kuhakikisha kila anayefanya fujo anakiona cha mtema kuni.
Tabaka la kwanza linajivunia silaha za jadi kama: Marungu, mawe na fimbo! Nalo tabaka la pili linatembea na zana za kisasa, mabunduki makubwa na mabomu kutoka bara Asia na Amerika yaliyonunuliwa kwa lengo moja tu – kushughulika na ‘watukutu’…

Post a Comment

 
Top