Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri Lukuvi.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaonya makampuni ya mawakala wanaoshughulika na kazi za kupiga minada nyumba na ardhi za watu mbalimbali kwa sababu tofauti zikiwemo madeni kwenye mabenki au mikopo mikubwa.Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Lukuvi amesema taratibu za kupiga mnada nyumba za wadaiwa lazima zifuate sheria na taratibu za nchi.Nitawafata niwaulize kwa nini wao wamenunua nyumba mbili, kwa nini mnada unafanyika Ijumaa saa 8? Halafu mtu anasimama na megafoni anajifanya kutangaza nyumba hii inauzwa… na tangazo moja limebandikwa kwenye ukuta… uongo mtu kumbe nyumba tayari imeshauzwa,” alisema Lukuvi.Aidha Lukuvi amewataka viongozi wa Mabaraza ya Ardhi kushughulikia kesi za migogoro ya ardhi haraka na mapema ili wahusika wapate haki zao na si kuwazungusha kila mara bila kutoa maamuzi kuhusu migogoro hiyo

Post a Comment

 
Top