Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Staa wa filamu Bongo, jina la Aunt Ezekiel Grayson akiwa na mpenzi wake mcheza dansa maarufu Bongo, Moses Iyobo ‘Moze’.
UKIAMBIWA utaje mastaa ‘grade one’ kunako kiwanda cha filamu Bongo, jina la Aunt Ezekiel Grayson haliwezi kukosa. Ni miongoni mwa mastaa wa kike katika tasnia hiyo anayetenda haki katika uhusika pindi anapokabidhiwa ‘scene’ na kama umebahatika kucheki filamu zake kama vile Mrembo Kikojozi, Yellow Banana, House Girl and House Boy, Nampenda Mke Wangu, Usiku wa Maajabu utaelewa namaanisha nini.Lakini pia mbali na uigizaji miaka kama mitatu iliyopita staa huyo aliingia kwenye uhusiano wa mapenzi na mcheza dansa maarufu Bongo, Moses Iyobo ‘Moze’ na hiyo ilikuwa mara tu baada ya aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte kutumikia kifungo nchini Dubai.
Akiwa na famili yake.
Aunt na Iyobo wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike waliompa jina la Cookie.
Over Ze Weekend imemtafuta Aunt kitaani kwake Kijitonyama jijini Dar ambapo katika makala haya amefunguka safari yake nzima ya maisha;
Over Ze Weekend: Mara nyingi mastaa huwa hawadumu na wapenzi lakini wewe na Iyobo mpaka sasa mna takribani miaka mitatu na miezi unaweza kutuambia siri ni nini?
Aunt: Kikubwa ni kuzungumza na moyo wako ulipotua ni mahali sahihi na je, unapata faraja unapokuwa hapo? Mi na Iyobo tunasikiliza sana.
Over Ze Weekend: Ni kitu gani kabisa ulikipenda kwa Iyobo?

Aunt: Unajua napenda sana mwanaume asiyekuwa na kero, asiyependa kuzungumza sana yaani kiufupi sipendi gubu, sasa kwa Iyobo vitu vyote hivyo hana.

Over Ze Weekend: Zamani ulikuwa gumzo kwa kubadilisha wanaume, mara Hatman, Silver, Joff na Jack Pemba nini kimekufanya ukaamua kutulia?

Aunt: Teknolojia sasa imekua, nimetulia na nina mtoto huyu Cookie (anamshika begani), anaweza kufungua kwenye mitandao na kumkuta mama yake ana skendo mbaya itakuwa siyo poa kabisa hivyo kila kitu kina wakati wake.

Over Ze Weekend: Unahisi kwa Iyobo umefika?

Aunt: Ndiyo, kwanza kabisa nasema hivyo kwa sababu kubwa amekuwa ni baba bora kwa mtoto wetu, mara nyingi nasikia malalamiko kwa baadhi

ya marafiki zangu kwa waume zao kutowajali watoto lakini mimi naweza kumuacha mtoto wangu na baba yake na nisiwe na wasiwasi hata kidogo.

Over Ze Weekend: Ikitokea aliyekuwa mumeo, Sunday akatokea na kuja kukuchukua kama mke wake wa zamani utafanyaje?

Aunt: Kisheria ya dini na hata kibinadamu nisingeweza kukaa muda huo ambao anatumikia kifungo na hata yeye mwenyewe alishawahi kuniambia hawezi kunilaumu kwa maamuzi yoyote ambayo ningechukua, kwa sababu hata alivyopata matatizo nilikuwa nikijaribu kuyashughulikia karibia mwaka mzima ndipo nikaendelea na mambo mengine.
Over Ze Weekend: Ulishawahi kupigwa hata kofi na Iyobo?
Aunt : Siyo kofi tu tunapigana kabisa lakini baadaye kama akigundua kama alinipiga kwa hasira basi anajirudi tunaombana msamaha na maisha yanaendelea.
Over Ze Weekend: Mara nyingi Iyobo, kazi zake ni za kusafiri na anakutana na watu mbalimbali hilo halileti shida kwenye uhusiano wenu?
Aunt: Yaah inasumbua sana mpaka kuna wakati unahisi unataka kushindwa lakini ukija hata kuangalia meseji anazotumiwa kupitia mitandaoni unagundua wazi kuwa wanampenda tu kwa sababu ni mtu f’lan.
Over Ze Weekend: Ulishawahi kumfumania Iyobo au yeye kukufumania?
Aunt: Nilishawahi kumfumania mara nyingi, na yeye alishawahi kubamba meseji kwenye simu yangu lakini inaonesha labda mtu alikuwa ananipenda na mimi nikampotezea na ishu kama hiyo ya kufumania ni lazima itokee hasa kwa sisi ambao tuna majina. Risasi: Kuna mipango ya kuolewa na Iyobo?Aunt: Hapana. Over Ze Weekend: Kwa nini wakati inaonekana mnapendana sana? Aunt: Unajua ishu ya ndoa ni mwanaume ndiyo anaamua kuoa mtu f’lan lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikubwa zaidi ni jinsi gani unaishi na mwenzako na mnaelewana kiasi gani.
Over Ze Weekend: Kwa kipindi ambacho upo na Iyobo hakuna ushawishi uliwahi kupata kutoka kwa mapedeshee mbalimbali?Aunt: Hata kama wapo sasa hivi siwezi kurubunika kwa sababu hakuna gari ambalo sijaendesha, viwanja ambavyo sijaenda na hela gani ambayo sijashika hivyo mwisho wa siku unaona yote ni mapito tu.
Over Ze Weekend: Mna mpango wa kuongeza mtoto mwingine?

AUNT: Ndiyo, mmoja lakini siyo kwa sasa hivi.

OVER ZE WEEKEND NA IMELDA MTEMA

Post a Comment

 
Top