Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Related image
TANGA: Rais Magufuli ameagiza Hakimu wa Mahakama ya Mazingara wilayani Handeni mkoani Tanga aliyetajwa kwa jina moja la Laizer ahamishwe mara moja kwa kushindwa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.Hayo ameyaagiza leo wakati akizungumza na wananchi wa Manga wilayani Handeni alipokuwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano mkoani humo.Wakitoa malalamiko yao,wakulima wa eneo hilo walimueleza Rais kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na wafugaji kwa kulishiwa mazao yao na wakipeleka malalamiko ya mahakamani hawapati haki zao..Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe alikiri kuwa, ni kweli hakimu huyo amekuwa hatendi haki, anapendelea upande mmoja wa wafugaji. hivyo kuwa kikwazo kikubwa kwa maendelo ya wakulima kwa kushindwa kutatua migogoro hiyo.

Post a Comment

 
Top