Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Agness Mmassy.
ALICHOKIFANYA MWANACHUO HUYU…
DaDa mmoja anayedai ni mwanafunzi wa chuo huko jijini Mwanza, agnes Mmassy, mkazi wa Singida, alichokifanya kimezua gumzo baada ya kutupia picha akiwa mtupu huku sehemu zake za siri akiziziba kwa taulo tu. Katika mitandao ya kijamii, picha hizo kila mmoja alizizungumzia kwa namna yake, baadhi wakisema ni laana, wengine wakidai hajitambui na ulimbukeni.
Risasi Jumamosi lilifanikiwa kuzungumza naye ambapo alikiri kuwa picha hizo ni zake na haoni tatizo lolote kuziweka mtandaoni. “Mimi ni Video Queen, sioni kama kuna tatizo, napenda kupiga picha za namna hiyo kwa sababu nataka kutengeneza jarida (magazine), hakuna mtu anayenishawishi bali napiga picha kwa sababu ninapenda kupiga picha hizo.
“Ninaishi na wazazi wangu wote na wanaona ni kawaida, kwa watu ambao zinawakera wala sijali kwa sababu furaha yangu ni kukaa hivyo kama walivyoona.
“Na picha hizi napigwa na mpigapicha mmoja, siyo kwamba nabadilisha na wala hatujawahi kushawishika kufanya tendo lolote baya zaidi ya kazi.“Mimi ni mwanachuo, niko mwaka wa kwanza na ninachukua Kozi ya Sheria, chuo kimoja kilichopo jijini Mwanza.
“Napata changamoto nyingi ila watu wajue kuwa siko kwa ajili ya mapenzi,” alisema msichana huyo.

Post a Comment

 
Top