Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ajali ilivyotokea, wananchi wakihamaki.
WANAFUNZI watatu wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya basi la abiria aina ya Coaster lililobeba wanafunzi na raia kugonga treni katika eneo la TANESCO, Morogoro Mjini.
Hali ilivyokuwa eneo la tukio.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri ambapo Coaster lilikuwa limebeba wanafunzi wengi wa Shule ya Sekondari ya Kayenzi waliokuwa wakienda shuleni pamoja na raia wachache lilipokatiza kwenye njia ya treni na kuligonga
Taharuki eneo la tukio.
Imeelezwa pia kuwa treni lililiibuiruza Coaster hiyo kwa umbali wa mita 30 kabla ya kusimama hivyo kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya Global Publishers.

Post a Comment

 
Top