Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Hali inazidi kuwa tmbaya katika nchi ya Venezuela baada ya kutokea machafuko wakati wa uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba uliosababisha vifo vya watu.
Waandamanaji wanaoipinga serikali ya rais Maduro wakiwa katika mapambano na polisi
Watu takribani 10 wanadaiwa kufariki dunia Jumapili hii katika maandamano hayo ambayo kati ya polisi wa nchi hiyo na waandamanaji wanaopinga Bunge hilo.
Polisi wa Venezuela wakiwa kwenye pikipiki wakati wa mapambano na waandamanaji
Rais Nicolas Maduro wan chi hiyo amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani ambao ndio wenye wabunge wengi katika bunge la Venezuela.
Mpaka sasa zaidi ya watu 100 wanakadiriwa kuuawa katika maandamano ya nchini humo ambayo yalianza kutokea takribani miezi minne iliyopita.

Post a Comment

 
Top