Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Amina Mpindogani.
Duniani kuna mambo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia simulizi ya kutisha, ya mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Amina Mpindogani (59), ambaye anakiri kwamba kwa muda mrefu, amekuwa akishiriki kwenye vitendo vya kishirikina, ikiwemo kula nyama za watu.
Akiombewa.
Global TV Online, imefanikiwa kukutana ana kwa ana na mwanamke huyo ambapo hapa anaanza kwa kujitambulisha:
Akipewa pongezi na mchungaji Marko Mzola wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu.
Lakini je, Amina alianza vipi kula nyama za watu? Akizungumza na Global TV, Amina alisema alianza kufundishwa uchawi na bibi yake (jina linahifadhiwa) tangu akiwa msichana mdogo lakini mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 50, baada ya kuona watu wengi wameanza kumshuku kuwa mchawi, alijiunga na chama cha waganga wa jadi ili kuwazuga waliokuwa wakimshuku mchawi.
Amina Mpindogani akifunguka na Global TV Online.
Baada ya kufanya mchezo hatari wa kula nyama za watu, kama ulivyomsikia mwenyewe, hatimaye Amina ameamua kuachana na uchawi na kumgeukia Mungu wake.
Matunguli yakichomwa moto.
Marko Mzola, ni mchungaji wa Kanisa la Hosana Ngome ya Yesu lililopo Nyakasangwe Msigani Kata ya Wazo jijini hapa ambapo yeye ndiye aliyempokea mwanamke huyo kwa mara ya kwanza na hapa anaeleza jinsi ilivyokuwa.
Matunguli yake.
Na hiyo ndiyo simulizi ya kutisha ya mwanamke huyu ambaye kama ulivyomsikia, amekiri kuhusika na ushirikina kwa miaka mingi, akila nyama za watu na jinsi alivyowatesa watu maishani kabla ya baadaye kumgeukia Mungu

Post a Comment

 
Top