Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Sharif Thabeet ‘Darassa’.
WAKALI wasioshikika kunako gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Sharif Thabeet ‘Darassa’ Jumamosi ijayo (Agosti 5) wanatarajiwa kuzindua hoteli ba’kubwa ijulikanayo kama JS Motel iliopo Chato Mjini mkoani Geita.
Msikie DarassaAkizungumza na mtandao huu, Darassa anayebamba na Ngoma ya Hasara Roho alisema kuwa, siku hiyo ataonesha burudani ya kutosha kutoka kwa wateja na waalikwa wote watakaofika katika uzinduzi.Huwa sikosei linapotokea suala la mualiko kama hili la uzinduzi. Nashukuru kuwa miongoni mwa watakaozindua JS Motel ndani ya Chato Mjini kwa mara ya kwanza na ninachoahidi kufanya makamuzi ya live jukwaani nikipiga nyimbo zangu zote ikiwemo Too Much, Sikati Tamaa, Weka Ngoma pamoja na ngoma yetu hii ya taifa ya Muziki,” alisema Darassa.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Shilole naye huyu hapa!
Kwa upande wa Shilole ama Shishi Baby kama wengi wanavyomuita alisema, siku hiyo ya uzinduzi atafanya tukio ambalo si la nchi hii kutokana na alivyojiandaa.
“Jumanne ijayo naachia ngoma yangu mpya inaitwa Kigoli lakini siku hiyo naenda kuzindua JS Motel nikiwa na ngoma mpya ya Kigoli na asikwambie mtu yaani nitakinukisha mwanzo mwisho, muziki wangu hakuna asiyeujua.
Siyo hiyo tu, nitawapa ladha ya ngoma zangu zote ikiwemo Hatutoi Kiki, Malele, Say My Name, Mtoto Mdogona nyingine kibao ambazo zitakuwa kama sapraiz,” alisema Shilole.

Post a Comment

 
Top