Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Esma Abdulkadiri na Hamad Manungwa ‘Petit Man’
NDOA ya mastaa wawili, Esma Abdulkadiri na Hamad Manungwa ‘Petit Man’ inadaiwa kuwa kwenye machafuko baada ya juzikati kuvuja madai kuwa, Petit alimfumania mkewe na jamaa mwingine, Risasi lina undani na ukweli wa habari hiyo.Chanzo ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake awali kilidai kuwa, wawili hao waliibua varangati la aina yake na kusababisha kufunga mtaa maeneo ya Tandale jijini Dar wanakoishi kutokana na kile kilichodaiwa ni Petitkumfuma Esma na mwanaume mwingine.Yaani ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kwani ilikuwa ni timbwili la aina yake baada ya Petit kudai amemfumania mkewe na mwanaume mwingine, hali iliyosababisha watu kibao kufurika pale wanapoishi Tandale,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Risasi Jumamosi lilianza kwa kumtafuta Esma ambaye kwanza aliangua kicheko kasha akasema kuwa anawashangaa watu wanaoeneza uvumi huo kwani kwenye maisha yake hajawahi kufumaniwa na haitatokea, isipokuwa ilitokea hali ya kutoelewana na watu kudhani alifumaniwa.Kugombana ni kawaida kwenye uhusiano lakini watu wanatakiwa kuuliza nini kimetokea siyo kuanza kuzusha maneno, ilikuwa ni kwenye bethidei ya B-12, sasa wakati tunakaribia kuondoka Petit Man alikuwa amelewa sana akawa anafanya fujo, sikupenda nikaamua kuondoka.
Alipofi ka nyumbani ikatokea ugomvi mkubwa akinilaumu kwa nini niliondoka nikamuacha kule, sasa yale makelele kwa jinsi tulivyokuwa tunazozana nahisi majirani walisikia wakaelewa tofauti na kueneza uvumi huo kwamba nilifumaniwa, ila tumeshayamaliza tupo sawa,” alisema Esma.
Kwa upande wake Petit Man alipotafutwa na kuulizwa kuhusu madai hayo ya kumfumania mkewe na mwanaume mwingine alisema: “Ni kweli ulitokea mtafaruku baina yetu lakini tumeshayamaliza haya mambo kifamilia.”

Post a Comment

 
Top