Friday, 21 April 2017

MSANII NIVA AWAPONDA WEMA SEPETU NA UWOYA KWA MKEWE


MUIGIZAJI wa kiume anayefanya vizuri Bongo, Zuberi Mohammed ‘Niva’ amefunguka kuwa hakuna mwanamke yeyote wa Bongo Muvi anayeweza kufi kia uzuri wa mkewe aitwaye Maisala, huku akiwaponda mastaa wakubwa kama Kajala Masanja,Wema Sepetu na Irene Uwoya. 

Akizungumzia maisha yake ya kindoa, Niva alisema anawashangaa wanaosema eti anaweza kumsaliti mkewe kwa kutembea na wasanii wa Bongo Muvi wakati aliamua kuoa kifaa ili atulie. 

“Nakuambia ukweli kabisa hakuna mwanamke mzuri Bongo Muvi zaidi ya mke wangu Maisala, wewe muamshe usingizini Uwoya, Wema, Kajala halafu muamshe na mke wangu uone nani anavutia zaidi, hakuna kama mke wangu,” alisema Niva.

About Author

Naveed Iqbal

Naveed is freelance web designer. He loves to play with javaScript and other programming codes.