Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba, Haji Manara kwenye Kamati ya Maadili baada ya kutoa maneno makali katika mkutano dhidi ya waandish wa habari juzi.
Sasa baada ya Manara kupata taarifa hizo kutoka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Mwenyewe ametaka mahojiano yake na kamati hiyo yarushwe LIVE.
Manara ameandika mtandaoni kwamba angependa mahojiano hayo kurushwa mubasharaa ili watu wajionee ni kitu gani watakacho muhoji na yeye atoe kile alichokuwa nacho akitumia lugha ya “kubutua”
Kwa mujibu wa alichoandika mtandaoni, inaonekana Manara hana imani na kamati hiyo pamoja na TFF iliyomfungulia mashitaka hayo.

Post a Comment

 
Top