WANAOMPINGA RAIS DONALD TRUMP WAPAMBANA NA POLISI

Watu 13 wamekamatwa huko Portland, Oregon, Marekani katika maandamano ya kumpinga rais Donald Trump yaliyogeuka kuwa mapambano na polisi.
Waandamanaji hao ambao walikuwa hawana kibali, walitapakaa katika mitaa nje ya majengo ya serikali ya Federesheni, na walikataa kutii tahadhari ya polisi.
Maandamano hayo ni miongoni ma maandamano machache yaliyofanyika Marekani ikiwa ni sehemu ya kampeni Siku ya ya 'Sio Rais Wangu' dhidi ya Trump.
       Polisi wakimdhibiti mmoja wa waandamanaji
     Mmoja wa waandamanaji akijikuta amewekwa mtu kati na polisi
   Na hapa muandamanaji akiwa amedakwa na polisi